AFUKUZWA NYUMBANI

 

Kijana Petro akiwa ndani ya Kanisa la Kirumba

Kijana Petro George anaekaa Ibanda amefukuzwa nyumbani mara baada ya kumwamini YESU katika Mahubiri ya Vijana yaliyofanyika Ibanda Mlimani.

Kijana huyu anaesoma katika Shule ya Sekondari Kabuhoro alimwamini Kristo katika Mahubiri hayo, mara baada ya kupokea ujumbe wa neno la MUNGU 

kutoka kwa Binti Juliana wanaesoma nae na kuamua Kubatizwa. Awali Kijana huyu amekuwa akisali katika Dhehebu la Anglikana. Akizungumza katika mahojiano yaliyofanywa na Mwandishi wa Habari hii kijana Petro alisema" Alipokea mwaliko wa kuhudhulia mahubiri ya Vijana kutoka kwa Dada Juliana 

na kuamua kuhudhulia ndipo aliposikia ujumbe wa neno la Mungu kutoka kwa Mwinjilisti Elton Mvanga na kukata shahuli kumfuata YESU".

Mama yake aliposikia hilo alimwambia "Atakapo amua kubatizwa tu! ndio mwisho wa maisha yake". Pamoja na Vitisho vyote hivyo kutoka kwa Mama na Baba yake mzazi. Kijana Petro akuogopa aliamua kubatizwa na kumkiri Bwana YESU. Alipo rudi nyumbani mara baada ya ubatizo, ndipo alipofukuzwa nyumbani na kuamua kuondoka 

 

Kijana Petro akibatizwa na Mchungaji Faustin Karuma.

kwa sasa Idara ya Vijana ya Mtaa wa Kirumba inamwangalia kijana huyu na kumtunza.

script type="text/javascript"> var _gaq = _gaq || []; _gaq.push(['_setAccount', 'UA-33516313-1']); _gaq.push(['_trackPageview']); (function() { var ga = document.createElement('script'); ga.type = 'text/javascript'; ga.async = true; ga.src = ('https:' == document.location.protocol ? 'https://ssl' : 'http://www') + '.google-analytics.com/ga.js'; var s = document.getElementsByTagName('script')[0]; s.parentNode.insertBefore(ga, s); })();