IDARA ZA KANISA NA UJUMBE WA MALAIKA WATATU
Kanisa la Waadventista Wasabato ulimwenguni linaongozwa na Idara mbalimbali ndani ya Kanisa.
Idara hizi zimewekwa ili kutekeleza ujumbe wa malaika watatu wa ufunuo 14;6-10; na "kuwaongoza watu kumkubali, kumpokea, na kumkiri Yesu kama Bwana na Mwokozi wao; na kuwaingiza katika kanisa lake; kuwatunza, na kuwaongoza katika kumshuhudia; na kuwaandaa kwa ajili ya kurudi kwake mara ya pili kunakokaribia"