HISTORIA FUPI YA IDARA YA HUDUMA ZA VIJANA:

  Katika hatua za uanzishwaji wa kanisa la Waadventista Wasabato halikuwa na muundo maalum wa huduma za vijana. Pamoja na ukweli kwamba vijana walikuwepo na walifanya kazi kubwa, kama vile James White alieanza kuhubiri na umri wa miaka 21, Ellen White alipata njozi yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka 17, John Loughborough aliyeanza kuhubiri akiwa na umri wa miaka 17.

Hawakuwa na muongozo wowote wa Idara ya Huduma za Vijana, bali walifanya kama walivyofanya watu wengine tu. Katika mpango wake mkuu "Bwana aliwachagua vijana kuwa mkono wake wa msaada".

Katika uhalisi wake uanzishwaji wa Idara ya huduma za Vijana hauwezi ukaelezeka vizuri bila kuwataja hawa Vijana wawili: Harry Fenner Umri wa miaka 17, na  Luther Warren Umri wa miaka 14 ambao katika mwaka 1879 walipiga magoti chini ya mti katika maeneo ya nyumbani mwao huko Hezelton Michigan wakimuomba Mungu jinsi wawezavyo kuwaleta vijana wenzao kwa Kristo.

Kama matokeo ya maombi vijana hawa wawili walianzisha umoja wa vijana tisa kwa ajili ya shughuli hiyo. Umoja huu waliouanzisha ulijulikana kwa jina la  Missionery Volunteer(MV) Mwaka 1891 umoja kama huu wa Hezelton, ulianzishwa huko Antigo Wisconsin. Hawa walikuwa na wanachama 30 chini ya uongozi wa Meade MacGuide. Mwaka 1892 Mama White alihimiza na kutia moyo vyama vya Vijana vilivyokuwa vimeanzishwa.

Mwaka 1901 Kanisa la Waadventista Wasabato katika Konferensi yake kuu ulimwenguni ilikipokea chama hiki na kuchukua hatua za awali za kuanzisha Idara ya huduma za Vijana. Kijana Luther Warren ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kwanza wa kamati hiyo. Kwa mara ya kwanza huduma za vijana zikaanza rasmi zikisimamiwa na Idara ya Shule ya Sabato. Katika miaka hii, ndo MV ilipoanzisha huduma za vijana wadogo (JMV) Missionary Volunteer.

Mwaka 1978 ndipo jina la " Idara ya Vijana " lilianza kutumika badala ya Missionary Volunteer

Miaka ya 1980  idara ya vijana ilijulikana kama AYO

Miaka ya 1990 jina lililojulikana lilikuwa AYS

Miaka ya 2000 jina lililotumika ni AY na Jina hili ndilo jina la Idara (Adventist Youth)

Chama cha mabalozi pia kilianzishwa mwaka 2001 ili kusaidia vijana wa umri wa kati kukabiliana na changamoto kubwa sana za maisha.

Hadi sasa Idara inaundwa na vyama vinne ambavyo ni:-

1. Adventurer  (Wavumbuzi) Miaka 6-9

2. Pathfinder (Watafutanjia) Miaka 10-15

3. Ambassador (Mabalozi) Miaka 16-21

4. AY. (Vijana wakubwa) Miaka 22-35++

 

 

 

  

 

 

 

 

 

 

script type="text/javascript"> var _gaq = _gaq || []; _gaq.push(['_setAccount', 'UA-33516313-1']); _gaq.push(['_trackPageview']); (function() { var ga = document.createElement('script'); ga.type = 'text/javascript'; ga.async = true; ga.src = ('https:' == document.location.protocol ? 'https://ssl' : 'http://www') + '.google-analytics.com/ga.js'; var s = document.getElementsByTagName('script')[0]; s.parentNode.insertBefore(ga, s); })();