Mahubiri ya Pr.Rudy yafurikisha Baraka tele Ziwa Victoria
MHUBIRI wa Kimataifa kutoka Canada ,Pr. Rudy Harnisch, ambaye alifanya mahubiri ya miezi miwili,Kirumba jijini Mwanza, mwaka jana, amefanikisha ujenzi wa makanisa matatu katika Mtaa wa Kirumba.
Pr. Rudy alichangia jumla ya shilingi milioni 18 ambazo zimetumika kuezeka makanisa hayo ya Jiwe kuu Mwanza, Chamabanda, na Ng’ombe B,wilayani Sengerema.Kanisa la Jiwe kuu
Upauzi wa makanisa hayo mawili ya Chamabanda na Ng’ombe B, katika wilaya ya Sengeema nje kidogo ya jiji la Mwanza umekamilika Machi mwaka huu wa 2012.
Kanisa ya Chamabanda
Kanisa la Ng’ombe B jinsi yanavyoonekana baada ya kupauliwa
Katika mahubiri hayo yaliyoongoa roho zaidi ya 200, wafadhili kadhaa walichangia jumla ya mabati 100 ambayo yamefaikisha upauzi wa Kanisa la Kabuhoro,jijini Mwanza. Mabati hayo 100 yana thamani ya shilingi 1,600,000.
Wakizungumza wakati wa kutenga kundi la Chamabanda kuwa kanisa kamili Machi 29 mwaka huu, Pr. Haston Mmamba ambaye ni Mkuu wa Mawasiliano wa Konferensi ya Nyanza Kusini(SNC)na Pr. Phaustine Karuma, ambaye ni Mchungaji wa Mtaa wa Kirumba, waliwahimiza washiriki wa makanisa hayo kutilia mkazo Misingi 28 ya Kanisa la Waadventista wa Sabato.
PR.Faustine Karuma(kushoto) na Pr. Haston Mamba(kulia) wakiwa mbele ya kanisa la Ng’ombe B
Wazee wa makanisa ya Chamabanda, Ng’ombe B na Kabuhoro katika picha ya pamoja na Mchungaji Mmamba na Mch. Karuma
Muinjilisti Elton Mvanga akisisitiza jambo wakati wa mahubiri huko Chamabanda. Mahubiri hayo yaliongoa roho zaidi ya 30
Wachungaji Mmamba(kushoto)na Karuma(kulia) wakimwekea mikono Mzee wa Kanisa la Chamabanda,Lameck Busagi
Picha ya pamoja ya Pr Karuma na Pr. Mmamba na washiriki wa kanisa la Chamabanda baada ya kutengwa kuwa kanisa kamili
Kanisa la Kabuhoro ambalo limejengwa kwa mabati.
Kutoka kushoto: Julius Kaitira, ambaye ni Mzee wa Kanisa kiongozi Kabuhoro, Mch. Karuma,Elisha Mwanzalima ambaye ni Mzee wa Kanisa la Kabuhoro na Fanuel Bigambo, Katibu wa Mtaa wa KIRUMBA Mkuu wa Majengo, Voronica Ernest, mbele ya kanisa hilo lililojengwa kwa mabati Machi 29 mwaka huu.