MAHURI YA MLIMANI JIJINI MWANZA YAANZA 

KANISA la Waadventista wa Sabato Kirumba, Jijini Mwanza, limeanza mahubiri ya majuma matatu katika eneo la Mlimani, Ibanda Juu.

Mahubiri hayo yamezinduliwa rasmi katika siku ya Jumapili, Mei 6 mwaka huu na Mchungaji Wilbert Nfubhusa, na yanatazamiwa kuwaleta watu mamia kwa Yesu.

Pr Wilbert Nfubhusa kushoto akishuhudia gwaride la ufunguzi wa mahubiri kulia ni Samweli Landiala mwenyekiti wa Mahubiri hayo.

Mch. Nfubhusa, ni Mchungaji kutoka Chato, katika Mkoa mpya wa Geita, katika Field ya Magharibi (West Tanzania Field) ambaye atakuwa mhubiri katika mahubiri hayo ya siku 21, yaliyo anza rasmi Jumapili,Mei 6.

Akihutubia katika viwanja vya Ibanda juu  Mch. Nfubhusa amesema, ujumbe mkuu wa mahubiri hayo ni kuwafanya watu wa Mungu waone haja ya kurudi kwa Baba, na watambue kwamba wamepotea mithili ya yule Mtoto Mpotevu.

 

 

Watafuta njia katika picha wakipiga gwaride wakati wa ufunguzi wa mahubiri .

Katika mahubiri hayo wamealikwa waimbaji wa Kwaya ya  Uinjilisti  Chato Misheni kutoka  Mkoa Mpya wa Geita, ambao uko katika Field ya West Tanzania, ambao tayari walikuwa wamewasili Jijini mwanza tangu Ijimaa ya Mei 4.

Katika mahubiri hayo pia yatafundishwa masomo ya Afya na Kaya na Familia na Maandiko Matakatifu kutoka katika Biblia. Pr. Nfubhusa, amesema huu ni wakati wa kupeleka UJUMBE WA MALAKA WA TATU.

Dunia ina jumla ya wakazi Bilioni saba, na kati yao bilioni moja ni Wakatoliki, milioni 500 ni Walokole kwa ujumla wao na Waadventista wa Sabato ni milioni 13.

Kufuatia hali iyo, Pr.Nfubusa amesema, wakati Wakatoliki ni 1/7 ya wakazi wote wa Dunia, tunapaswa kuhubiri kwa nguvu na kwa haraka,ili kuupeleka ujumbe wa ONYO LA MWISHO kwa Ulimwengu,katika wakati huu wa kufungwa kwa historia ya Ulimwengu.

Hadhira, ama wasikilizaji katika viwanja vya Ibanda Mlimani

 

 

Picha baadhi ya wasikilizaji waliojitoa kumpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wao

             Agape Voice wa Jijini Mwanza, walitikisa Bonde la Ufa la Kenya View more

 

script type="text/javascript"> var _gaq = _gaq || []; _gaq.push(['_setAccount', 'UA-33516313-1']); _gaq.push(['_trackPageview']); (function() { var ga = document.createElement('script'); ga.type = 'text/javascript'; ga.async = true; ga.src = ('https:' == document.location.protocol ? 'https://ssl' : 'http://www') + '.google-analytics.com/ga.js'; var s = document.getElementsByTagName('script')[0]; s.parentNode.insertBefore(ga, s); })();