KIRUMBA ADVENTIST CHOIR  ( K.A.C)

Kwaya kongwe ya Wasabato 

Tarehe 21/04/2012

 Kirumba Adventist Choir (K.A.C) ilianzishwa mnamo mwaka 1965.

 Ni moja ya kwaya kongwe katika Ukanda wa Ziwa na katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mtu anaweza kuimba; lakini uimbaji ni sayansi yenye kupanga sauti kwa kutumia mfumo halisi wa Staff NOTATION, ama noti.

Katika kwaya hii, kuna waimbaji wenye vipaji na mabingwa wa kutunga nyimbo kwa kutumia sayansi hii. Unaweza kusema, Kirumba Kwaya,kuna magwiji halisi wa muziki wa Injili, na muziki wao huandikwa kwa kutumia sayansi halisi,kulingana na taaluma ya muziki.

Washiriki wengi wa kanisa la Wasabato hapa nchini, wamewahi kusikiliza nyimbo zao nzuri katika kanda za sauti na picha?. Ama, Watanzania na wana Jumuiya ya Afrika Mashariki, hawajawahi kusikia mirindimo ya Injili ya kwaya hii mahiri?

 Kwaya  hii imemea mithili ya mmea na ilipofika mwaka wa 1968   ilikuwa chini ya  Hayati   Josiah Paul Sagati, ambaye ni mwalimu nguli wa muziki wa injili  aliifundisha kwaya ya Kirumba hadi alipofariki, mwaka 2007.

 Walimu wengine ni pamoja na Patroba Maginga, Mr. Darlington Onditi,  Mw. Kondi, Innocent Mujaya, Ahadi J. Sagati, Amosi Omary, John Kanyara, Herode Kazagata, Edward E. Magori, Pactamed Mwijarubi, Pascal Vedastus na John Kanagana.

Mwalimu Patroba Ndege Maginga

 Baadhi ya waimbaji wa kwanza ni pamoja na Mrs. Mziba, Neema Gideon, Anna Maganda, Martha Bomani, Winner Reuben, Chimoro Josiah, Benda Nyang’araga, Stella Mwamkonda, Eliabu Mashauri, Ruth Mbwambo, Joushua Mulla, Giliadi Mambo, Eliabu Mashauri, Andrew Magoma, n.k na kwaya ikiwa chini ya wazee wa kanisa Mr. Martin Buguzi, Petro Kazi na mzee Mulla, wote hao wakiongozwa na Mch. Mwakalinga, Mch. Onyango.

Kwaya hii ni miongoni mwa kwaya kongwe hapa nchini na katika Kanda ya Ziwa ilikuwa kwaya ya kwanza ya ki-Kristo kurekodi nyimbo za injili mwaka 1982; ikifuatiwa na A.I.C Makongoro.

 Kwaya iliendelea kufanya kazi ya injili na kutoa senturi mbalimbali. Na ilipofika mwaka 2005 ilifanikiwa kutoa mkanda wa kwanza wa video; na mwaka 2006 ikatoa mkanda wa pili.Kanda hizi ni WENGI WANA RAHA,na YEYE TUMAINI LANGU.

Kwaya imeshafanya uinjilisti wa nyimbo kupitia mikutano ya injili (mahubiri), matamasha huduma kwa jamii katika vituo mbalimbali vya hapa nchini, hata hivyo kwaya imekuwa na safari kadhaa za nje ya nchi.

Hadi sasa kwaya ina waimbaji 45 chini ya mwalimu Dr. Darlington Onditi, Paschal Vedastus  na Mwenyekiti Mr. Nicolaus  Mujaya.

*Msafiri Paul ni Katibu wa Kwaya

 

 

script type="text/javascript"> var _gaq = _gaq || []; _gaq.push(['_setAccount', 'UA-33516313-1']); _gaq.push(['_trackPageview']); (function() { var ga = document.createElement('script'); ga.type = 'text/javascript'; ga.async = true; ga.src = ('https:' == document.location.protocol ? 'https://ssl' : 'http://www') + '.google-analytics.com/ga.js'; var s = document.getElementsByTagName('script')[0]; s.parentNode.insertBefore(ga, s); })();