Agape Voice wa Jijini Mwanza, walitikisa Bonde la Ufa la Kenya

WAIMBAJI wa Kundi mahiri la Agape Voice la Jijini Mwanza, wameshiriki mahubiri ya majuma mawili Mkoani Rift Valley, nchini Kenya yaliyoanza Mei Pili hadi 12 mwaka huu 2012

 

  Agape Voice wakiwa katika Chuo Kikuu cha Egerton,Nakuru,Kenya.

Mahubiri hayo yaliendeshwa na Muinjilisti Daniel Machango, katika kitongoji cha Chepareria, huko West Pokot, ambako watu 32 walibatizwa.

 Mkuu wa Kundi la Agape,Lillian  Jonathan,amesema walifanya kile ambacho walimwomba Mungu wakifanye.

 Wakiwa Rift Valley, walishiriki mahubiri hayo kwa kutembelea watu na kuwaalika katika mikutano ya Injili, wakati huohuo walishiriki kuwaombea watu mbalimbali wa kitongoji  hicho cha Chepareria.

Agape Voice: Kutoka kushoto; Misso Yusto,Afra Masinde, Evarine Adwerk na Lillian Jonathan Bomani.

Hii ni mara ya pili kwa kundi hili kuzulu nchini Kenya kushiriki mikutano ya Injili. Desemba mwaka jana kundi hili lilikwenda nchini Kenya, mjini Nakuru kuimba katika Mkutano wa Injili katika kitongoji cha Beeston, ambako watu wanne walibatizwa.

Kulingana na Lilian Jonathan, Agape wakiwa nchini Kenya, walifanya Huduma za Jamii kama kuwapa wahitaji chakula,mavazi na vitabu vya Roho ya Unabii.

Muinjilisti Daniel Machango akihubiri huko Chepareria, West Pokot,Rift Valley,KENYA.

Mahubiri ambayo AGAPE VOICE wamekuwa wakihudhuria nchini Kenya, yamekuwa yakiendeshwa  na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Egaton,cha nchini Kenya wakati wa likizo.

Agape Voice: Afra Masinde, Lillian Jonathan  na mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Egerton,Beverlyn Ochieng(kulia) walipokwenda kumpa huduma  Bi.Lillian Chuma  aliyekuwa amejifungua,lakini katika hali ya kuhitaji msaada.

 

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Egerton,  wakijenga kanisa kwa ajili ya Tawi la Shule ya Sabato.

 

Hadhira, ama wasikilizaji katika viwanja vya Mahubiri katika kitongoji cha Chepareria.

Back to home page 

 

 

script type="text/javascript"> var _gaq = _gaq || []; _gaq.push(['_setAccount', 'UA-33516313-1']); _gaq.push(['_trackPageview']); (function() { var ga = document.createElement('script'); ga.type = 'text/javascript'; ga.async = true; ga.src = ('https:' == document.location.protocol ? 'https://ssl' : 'http://www') + '.google-analytics.com/ga.js'; var s = document.getElementsByTagName('script')[0]; s.parentNode.insertBefore(ga, s); })();