TOVUTI YA KANISA LA KIRUMBA YAZINDULIWA RASMI:

Pr Aston Mmamba katika picha akisisitiza umuhimu wa kutumia teknohama kanisani.
MKUU WA MAWASILINO wa Kanisa la Waadventista wa Sabato katika Jimbo la South Nyanza, Pr Aston Mmamba, amesema umefika wakati kwa makanisa kutumia nyenzo za mawasiliano za kisasa kutangaza Ujumbe wa Malaka wa Tatu.

Akizungumza wakati wa kuzindua rasmi tovuti ya Kanisa la Kirumba,Jijini Mwanza, Jumamosi, Aprili 28 mwaka huu, Mch. Mmamba amesema Idara ya Mawasiano kanisani njozi yake ni kujenga taswira njema ya kanisa.

“Utume wake ni kujenga madaraja ya matumaini…wako watu sasa hawana matumaini kwa Mungu. Hawa wote ambao madaraja yao yamevunjika, wanapaswa kurejeshewa matumaini,ili wamwawini Kristo”,Mch.Mmamba amesema.

Amesisita, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEKNOHAMA) kama simu za mkononi na kompyuta zenye kutoa fursa pana na mitandao ya kijamii kama  Facebook ,tovuti na  brogu, zitasaidia kupeleka Ujumbe wa Marejeo ya Kristo kwa watu .

Tovuti ya Kanisa la Waadventista Kirumba, imeanzishwa miezi michache iliyopita, na imesheheni habari,mahubiri,mafundisho anuwai na matangazo ya kanisa, na inategemewa kuweka daraja kati yake na watu wengi waishio ndani nanje ya nchi.

Mch.Mmamba amewataka Waadventista wa Sabato kutangaza sura njema ya Kanisa letu na taasisi zetu kama shule,zahanati,hospitali n.k.  kupitia TEKNOHAMA.

Idara ya Mawasiliano inapaswa kutoa habari kwa umma, kwa kuwa visa na vituko vyenye kutia moyo katika Kazi ya MUNGU havijapata kutangazwa.

“Kazi ya Mungu hata kama ni kuombea wagonjwa,wakiwemo wenye mapepo na wagonjwa wasioweza, hazitangazwi kwa umma wapate kumjua Kristo”, Mch. Mmamba alisisitiza.

“Habari na taarifa lazima kuibuliwa na kutangazwa, ili zijulikane na watu wengine. Umma unapaswa pia kujua mahali makanisa yetu yalipo, na kutagaza habari na taarifa sahihi zinazojenga taswira njema kwa kanisa,ili kujenga mahusiano mazuri kwa serikali,raia na jamii.”Alisema, huku akisisitiza kwamba mahubiri na majuma ya maombi katika nchi anuwai leo huendeshwa kwa kutumia Njia hizi za kisasa za mawasiliano.

Mkuu wa mawasiliano Mr Samwel Nkonya akisikiliza hotuba ya

Pr Aston Mmamba wakati wa uzinduzi wa tovuti ya Kanisa la Kirumba.

script type="text/javascript"> var _gaq = _gaq || []; _gaq.push(['_setAccount', 'UA-33516313-1']); _gaq.push(['_trackPageview']); (function() { var ga = document.createElement('script'); ga.type = 'text/javascript'; ga.async = true; ga.src = ('https:' == document.location.protocol ? 'https://ssl' : 'http://www') + '.google-analytics.com/ga.js'; var s = document.getElementsByTagName('script')[0]; s.parentNode.insertBefore(ga, s); })();