UZINDUZI WA PROGRAM YA KAYA NA FAMILIA: TAREHE 21/04/2012
Idara ya Kaya na Familia katika kanisa la Kirumba imezindua program kabambe ya kuboresha kaya na familia zetu. Akizungumza katika program hiyo mkuu wa Idara hiyo Mzee Venerable Mziba, alisema; “Kaya na Familia ndicho kiini cha Kanisa na Kanisa aliwezi kukua kama familia zetu zitakuwa na migogoro, alisisitiza kulejesha upendo kwa wanandoa”. Alinukuu kutoka katika kitabu cha Ezekieli 16:8, Basi, nilipopita karibu nawe, nikakutazama; tazama, wakati wako ulikuwa wakati wa upendo; nikatandika upindo wa vazi langu juu yako, nikakufunika uchi wako; naam, nalikuapia, nikafanya agano nawe, asema Bwana MUNGU, ukawa wangu.
Katika uzinduzi huo washiriki walipata fursa ya kugawanyika katika vikundi kulingana na jinsia zao na kujadili changamoto mbalimbali zinazokabili familia zao. Baada ya kujadiliana waliwasilisha hoja mbalimbali kwa mkuu wa Kaya na Familia ili ziweze kufanyiwa kazi.
Katika program hiyo washiriki walifurahia namna ilivyoandaliwa na kupangiliwa na walipendekeza kuwa Idara iyandae program kama hiyo ili kupata mrejesho wa changamoto hizo.
Mr na Mrs Venerable Mziba, wakiwa katika picha ya pamoja.