CHATO ADVENTIST MISSION YAFANYA MAKUBWA JIJINI MWANZA
Kwaya ya Chato Adventist Mission imefanya makubwa katika jiji la Mwanza. Kwaya hii ambao ni mara ya kwanza kuja katika jiji hili la Mwanza, ilialikwa na Kanisa la Kirumba Adventist kuja kuhudumu katika mahubiri ya wiki tatu. Katika mahubiri hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Ibanda juu yakiongozwa na Pr Wilbert Nfubhusa pamoja na kwaya hii, jumla ya watu 102 walimpokea Yesu na kubatizwa. Akizungumza katika kuhitimisha mahubiri hayo, mchungaji Karuma alisema "Kwaya ya Chato mission ni kwaya ya uinjilisti kwani inauhakika na kile inachokifanya katika kumtumikia Bwana". Kwaya hii imetumika sehemu mbalimbali na watu wengi wamempokea Yesu na kubatizwa. Katika kuhitimisha mahubiri hayo kwaya hii ilizindua albamu yake ya kwanza yenye jina la SITA RUDI NYUMA na kufanikiwa kupata pesa za kitanzania milioni mbili na laki mbili.
Baadhi ya washiriki wakizungumza baada ya uzinduzi huo walisema " Ili tutimize ujumbe wa malaika watatu imefika wakati ambapo kwaya zetu zinapaswa kujitoa kama kwaya hii. Katika uzinduzi huo wana wa kike wa Kanisa la Waadventista Wasabato Kirumba waliwapatia zawadi kila mwimbaji mmoja mmoja na kuhitimisha kwa kumpatia zawadi Pr Wilibert Nfubhusa na mwenyeji wake Pr Faustin Karuma.