KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO KIRUMBA WANUNUA KANISA
Kanisa la Waadventista Kirumba, jijini Mwanza, limenunua jengo lenye thamani ya shilingi Milioni 17 ili kwa ajili ya kundi lake la Ghana
Mkuu wa Mawasiliano wa Kanisa la Kirumba, Samuel Nkonya, amesema jengo hilo lililoko maeneo ya Green View, jijini Mwanza, litavunjwa ili kanisa jipya lipate kujengwa baadaye.
Awali, jengo hilo(pichani) lilikuwa nyumba ya kuuzia vileo(bar) na sasa litatakaswa na kuwekwa wakfu kwa ajili ya kuwa Nyumba ya MUNGU aliye hai.