RADIO YA MORNINGSTAR YAZINDULIWA RASMI MWANZA:


Radio ya kanisa la Waadventista Wasabato Morning Star imezinduliwa rasmi leo Katika kanisa la Waadventista wa Sabato Kirumba na Pr Mussa Mika ambaye ni mkurungezi wa mawasiliano wa Tanzania union.

 Pr Mussa Mika kulia akitoa somo wakatika wa ibada 

kushoto ni mkuu wa maswasiliano wa kanisa la Kirumba Mr Samwel Nkonya.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mchungaji Mika amesema kuwa “Sasa Kanisa la Waadventista wa Sabato linazidi kupaa na kuutangaza ujumbe wa Malaika watatu". Amewataka Washiriki wa kanisa kuiambia Dunia kuwa ujumbe tulionao ni wa kweli na hakika na kutumia njia zote za mawasiliano hasa katika wakati huu wa utandawazi. Alikazia kuwa agenda ya kanisa ni kumwinua Mungu, kumsifu na Kumtangaza kwa watu wote.

Nae mtaalamu wa maswala ya ufundi kutoka Hope Channel Mr Enoch Mogusu amesema kanisa limejipanga vizuri sana katika kuahakikisha kuwa radio hii inasikika katika mikoa kumi ya Tanzania bara haraka iwezekano. 

 

Mr  Enoch Mogusu Mtaalamu wa ufundi kutoka Hope Channel.

Wakizungumza kwa furaha baada ya uzinduzi huo Washiriki wa kanisa la Kirumba wamesema wamekuwa wakingojea sana radio hii na sasa itatimiza matarajio yao kwa ulimwengu huu uliochoka.

Pia washiriki wameuomba uongozi wa Tanzania union kuhakikisha kuwa unafanya kila limezekalo ili kuwepo na kituo hapa Mwanza cha kurusha na kuandaa vipindi.

script type="text/javascript"> var _gaq = _gaq || []; _gaq.push(['_setAccount', 'UA-33516313-1']); _gaq.push(['_trackPageview']); (function() { var ga = document.createElement('script'); ga.type = 'text/javascript'; ga.async = true; ga.src = ('https:' == document.location.protocol ? 'https://ssl' : 'http://www') + '.google-analytics.com/ga.js'; var s = document.getElementsByTagName('script')[0]; s.parentNode.insertBefore(ga, s); })();