24 WABATIZWA KATIKA MAHUBIRI MLIMANI KIRUMBA:
JUMLA ya waumini wapya 24 wameongoka na kubatizwa kufuatia mahubiri yaliyomalizika Jumamosi, Julai 7 mwaka huu, huko Ibanda, Mlimani jijini Mwanza.
Mahubiri hayo yaliyodhaminiwa na Idara ya Vijana wa Mtaa wa Kirumba, yaliendeshwa na Munjilisti Elton Mvanga kwa majuma mawili
Mzee wa Kanisa la Kirumba,Charles Malunde, amesema kwa wastani watu 50 walikuwa wakihudhuria katika mahubiri hayo kila siku; kwa hiyo watu 24 waliobatizwa katika mahubiri hayo ni asilimia 50 ya mahudhurio.
Katika mahurihi hayo, kulikuwa na vipindi vya mafundisho ya usiku pamoja na Sinema.
Muinjilisti Elton Mvanga, aliyeendesha mahubiri ya Vijana, Mlimani Ibanda(pichani)
Waongofu hao walibatizwa Ijumaa,Julai 6 kanisani Kirumba na Mchungaji Faustine Karuma; wakati wawili waliojitoa watabatizwa wakati wa Mkutano wa Makambi utakao anza Julai 29 mwaka huu.
Baadhi ya Picha za waliobatizwa siku hiyo.